kwamamaza 7

Wakimbizi 22 asili ya DR Congo wahukumiwa tena kufungwa mwezi kizuizini

0

Mahakama kuu ya Muhanga,kusini mwa Rwanda leo tarehe 26  Aprili 2018 imehukumu kuwafunga jela mwezi kizuizini wakimbizi 22 asili ya DR Congo juu ya mashtaka ya kuandamana kambini,vitendo vya ugaidi,kupambana na maafisa wa usalama na kudharau sheria za Rwanda.

Mahakama imeamua hili baada ya ombi la mwendeshamashtaka la kuongeza siku 30 za kuwafunga ili wasifungwe kinyume na sheria.

Wanasheria wa washtakiwa Me Alice Mulisa na Gilbert Ndayambaje wamesema wateja wao wangeliachiwa huru kwani walisha fungwa siku 30 na wameongeza mwendeshamashtaka alimaliza upelelezi wake kwa hiyo watuhumiwa wanastahili kuachiwa huru.

Washtakiwa wamekanusha mashtaka yote na kuomba kuachiwa huru.

Mahakama itahukumu kesi hii tarehe 30 Aprili 2018.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.