kwamamaza 7

Wake wa marais warembo zaidi barani Afrika [Tazama mapicha]

1

Katika kila taifa, nidhamu na mavazi ya mke wa rais ni muhimu na huigwa sana. Yaani ndiye picha ya nchi kwa njia nyingine. Japo wao utofautiana katika hulka na kimaumbile, wote huzingatia sana maadili na tamaduni za nchi. Mtandao wa Bwiza.com umekupa wake wa marais wa Afrika ambao wanatamanika sana kwa urembo wao.

 1. Malkia Lalla Salma (Morocco)

malkia-lalla-salma-morocco

Malkia Lalla Salma ni mke wa mfalme wa nchi ya Morroco, Mohammed wa sita. Ndiye mke wa mfalme wa kwanza kutambulika sana na kupewa jina la kifalme.  Ana shahada ya uhandisi na ni mzazi wa watoto watatu.

 1. Sylvia Bongo Ondimba (Gabon)

sylvia-bongo-ondimba-gabon

Sylvia Bongo Ondimba  alikuwa mke wa rais tangu mwaka wa 2009 baada ya mume wake kuingia mamlakani. Anatambulikana pia kama mmoja wa wake wa rais warembo sana duniani. Anajulikana kwa kumakinika kwake na mavazi ya kisasa.

 1. Chantal Biya (Cameroon)

chantal-biya-cameroon

Anasifika kwa mtindo wake maarufu wa kusonga nywele. Hupenda rangi kali ambazo humfanya kuonekana kwa mbali na katikati ya umati, jambo ambalo halimuogopeshi hata kidogo.

 1. Hinda Deby Itno (Chad)

hinda-deby-itno-chad

Anajulikana sana kwa sahihi yake yenye urembo mwingi. Hinda huandamana na mumewe katika hafla zote za kijamii. Pia, ni katibu wa kipekee katika kamati kuu ya mawaziri wa rais. Inasemekana rais wa Chad alisema kuwa Hinda humsaidia katika usimamizi wa taifa. Kwa wanawake wengi wa Chad, Hinda huwa ni mfano wa kuigwa.

 1. Zeinab Suma Jammeh (Gambia)

zeinab-suma-jammeh-gambia

Ni mwenye asili ya Morocco. Maadui wake humuita shetani au mfuata pesa. Ni mama wa watoto wawili. Yakumbukwa kwamba alihamia Marekani baada ya mumewe kutangaza kumwoa Alima Sallah aliyekuwa na umri wa miaka kumi na minane. Hiyo ilimfanya Jammeh kumtalaki Alima japo hakuna ushahidi halisi kwamba waliachana na huyo mke wa pili.

 1. Margaret Gakuo Kenyatta (Kenya)

margaret-gakuo-kenyatta-kenya

Ni mke wa Rais wanne wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Japo amefikisha miaka hamsini, urembo wake na mtindo wake wa nywele hupendeza sana. Yeye hupenda kukaa maisha ya kawaida tu. Hapendi kuongea sana na hivyo watu humwona kama mwenye haya sana.

 1. Malkia Inkhosikati LaMbikiza (Swaziland)

queen-inkhosikati-lambikiza-swaziland

Ni mke wa kwanza wa Mfalme Mswati wa tatu kujichagulia kwani wale wengine kumi na wane ni walichaguliwa. La Mbikiza akiwa na miaka kumi na sita, alitoroka shuleni aoelewe na mfalme. Baadaye alienda kusomea shahada ya sharia japo kwa sasa haifanyi kama kazi yake akiogopa kuonekana akipendelewa kwa kuwa mke wa mfalme.

 1. Ana Paula dos Santos (Angola)

ana-paula-dos-santos-angola

Kabla ya kuolewa na Rais, Anna Paula alikuwa mhudumu wa ndege.  Alikutana mpenzi wake katika mojawapo ya ndege za rais alimokuwa anasafiria. Ni mama wa watoto watatu akiwa na shahada ya sharia na ualimu. Alianzisha shirika la kutetea wanyonge, hasa wanawake na watoto.

@Bwiza.com

1 Comment
 1. Dylan Larkin Jersey says

  Because you currently have many finance commitments like repaying your financial troubles plus home loan, in addition to finding cash for your own personal kids’ institution – it is advisable to own substantial cost to help ease fiscal pressure. In fact , every single amount of cash that you choose to receive or receive has it has the affect defeating the economic recession. For that reason your company’s savings and also emergency money are needed to prepare in the worse yet that would arise during poor situations. under $2000, and quite possibly borrow these income through certain mortgage financial institutions.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.