kwamamaza 7

Wake milioni 5 watauawa na saratani mnamo 2030-utafiti

0

Utafiti wa shirika la Marekani la kuchunguza shughuli za maisha, Global Health, ulionyesha katika ripoti ilitolewa jana kwamba waathirika wa ugonjwa wa saratani umeongezeka kwa kiwango cha 60 %; na kutakuwa na vifo vya wanawake takribani milioni tano mnamo mwaka wa 2030.

Ugonjwa wa saratani huwauwa wanawake 14% kila mwaka na utafiti kuhusu ugonjwa huu unaripoti kwamba nchi mbali mbali mithili ya Danmark huonyesha kukabiliwa na saratani kwa kiwango cha juu.

Utafiti ulionyesha kwamba maskini ndio wanaokabiliwa na ugonjwa wa saratani kuliko matajiri na pengine wanawake vijana hukabiliwa sana kuliko maajuza.

[ad id=”72″]

Kiongozi makamu wa Global Health, Sally Cowal alisema kwamba ugonjwa wa saratani unawazidisha raia uwezo wa kujikinga kwani huwauwa kwa wingi wanaokosa namna ya kutibiwa.

Sehemu zinazokabiliwa zaidi ni mapafu, matiti, ubongo na sehemu nyinine na mgonjwa wa saratani anaweza kupona wakati imejurikana mapema na kutibiwa vizuri.

Shirika la kimataifa la utafiti juu ya ugonjwa wa saratani linasema kwamba mnamo 2012 kulikuwa na wagonjwa milioni 6.7 duniani; na wanawake milioni 3.5 walifariki kwa ajili ya ugonjwa huo.

[ad id=”72″]

Wathirika wengi hupatikana katika bara la Ulaya, Asia na nchi zinazojitahidi kufikia maendeleo. Katika nchi za barani Afrika, waathirika wengi hupatikana Zimbabwe, Malawi na Kenya.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.