[ad id=”72″]

Kwa sasa kundi ambalo linalojiita Dola la Kiislamu limejisema kuhusika na shambulio mjini Berlin lilifanywa jumatatu.

Wakati huo huo polisi ya Ujerumani imeongeza juhudi za kumsaka dereva wa lori ambalo lilitumika kushambulia soko la Krismas mjini humo, katika shambulio baya lililotokea siku ya Jumatatu.

Mtuhumiwa pekee Mpakistani anayeomba hifadhi nchini Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 ,aliachiwa huru jana jioni kwa kukosa ushahidi, na hatua hiyo imesababisha wasi wasi kwamba mtu aliyehusika na shambulio hilo bado yuko huru.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere alikiambia kituo cha televisheni cha Ujerumani ZDF kwamba haondoi uwezekano kwamba mtu aliyefanya shambulio hilo bado amejificha.

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck akizungumza katika misa ya kuwakumbuka wahanga , alisema lengo la shambulio hilo ni kuwafanya Wajerumani wawe katika hali ya kuogopa.

Kwa mujibu wa waziri De Maiziere watu 24 ambao wamejeruhiwa wanaendelea kuwapo hospitali , 14 kati yao wako katika hali mbaya.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.