kwamamaza 7

Wagombea Urais walalamikia ratiba ya uendeshaji kampeni iliyowekwa NEC

0

Baadi ya waliotangaza nia yao ya kugombea urais wanaonyesha wasiwasi dhidi ya ratiba ya kuendesha kampeni waliyowekewa na NEC.

Kamati ya Uchaguzi ya Rwanda yasema kuwa muda wa kuendesha kampeni ambao wagombea urais waliowekewa ni wakutusha huku wakitarajiwa kuanza kampeni zao kutoka tarehe ya 14/7 hadi 03/8. Kwa hiyi wagombea watalazimika kufanya ziara za kampeni zao mnamo siku 19 ambako watalazimika kufika angalau wilaya mbili kwa siku ikiwa wanapanga kufikia wilaya zote.

Dkt. Frank Habineza, mgombea kwa tiketi ya Democratic Green Party of Rwanda, asema kuwa kulingana na muda mchache waliopewa wa kuendesha kampeni zao watalazimika kufika wilaya mbili kwa siku na anaona itakuwa vigumu.

“Tumekuwa tukifikilia kwenda nchi za ng’ambo kama Marekani, Ubelgiji na Uingereza kuwakuta wapiga kura wa diaspora ila kwa uchache wa muda tuliopewa nadhani haitawezekana” Aliendelea kusema

Kwa upande wa Mwenedata Girbert,mgombea binafsi, asema kuwa wakati usiofika hata mwezi waliowekewa ni mchache kufikia nchini kote.

Kwa kweli si rahisi hata kidogo lakini tutafikilia la kufanya. Hatutegemei mabadiliko ya ratiba ya Uchaguzi bali tu ingekuwa bora kukiwekewa muda zaidi ya mwezi kwa ajili ya kampeni” Alisema

Charles Munyaneza, Katibu Mtendaji wa Kamati ya Uchaguzi (NEC) amesema kwa kujibu malalamiko haya, kwa mjibu wa habari kutoka The New Times, kwamba siku 19 zilizowekwa ni muda wa kutosha ilimradi wagombea wametayarisha shughuli zao za kampeni awali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Hii si mara ya kwanza kukifanyika kampeni uchaguzi wa rais kwa muda sawa na huyu na hatukukuta tatizo lolote. Licha ya hiyo pia Rwanda si nchi kubwa kwamba mgombea hataweza kufika wilaya moja kwa saa za asubuhi na kwenda nyingine saa za mchana na akamaliza shughuli zake kabla ya saa 6: 30. Wanachotakiwa ni kutayarisha shughuli zao kulingana na sheria.”

Katibu huyo alisema pia kwamba licha ya hayo yote shughuli za nchi hazitasimama, kwamba wanyarwanda wanataka muda wa kufanya shughuli zao za kibinafsi na si kupoteza muda wao wote kwa kushiriki kampeni.

Charles Munyaneza aliwahimiza pia kutumia vyombo vya habari kwa kuendesha kampeni zao, pia na kutumia wawakilishi wao ili kuendesha kampeni kwa nafasi yao.

Juhudi za kuasilisha nyaraka za wagombea kwa NEC zilizoanza tarehe 12 zinaendelea, huku wagombea 3 wakiwa wamekwisha asilisha nyaraka zao akiwemo Mweneda Gilbert, Barafinda Fred na Frank Habineza wa Green Party.

Tarehe ya mwisho ya kuasilisha nyaraka ni 27/6 na wagombea rasmi kutangazwa tarehe 07/07. Kunasubiriwa nyaraka za wagombea Shimwa Rwigara Diane na Mpayimana Philippe ambao wametangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi wa hapo mwezi Agosti.

Ikumbukwe pia kwamba rais Paul Kagame atakuwa mgombea huku akiwania muhula wa tatu na inategemewa kuwa ndie mshindi wa uchaguzi huu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.