Swahili
Home » Wafanyabiashara wa mpaka wa Rubavu/Goma waomba kuwekwa chapa ya orodha ya bidhaa zenye kutozwa ushuru wa forodha
BIASHARA HABARI MPYA

Wafanyabiashara wa mpaka wa Rubavu/Goma waomba kuwekwa chapa ya orodha ya bidhaa zenye kutozwa ushuru wa forodha

Biashara ya kuvuka mpaka haijakuwa rahisi kuendeshwa licha ya kwamba mawaziri wa nchi ya Rwanda na DRC walisaini mkataba wa kurahisisha biashara kati ya wafanyabiashara wadogo wa kuvuka mpaka.

Wafanyabiashara hawa wanasema kwamba wanazikuta bado pingamizi kadhaa za ulipaji ushuru kwa bidhaa zote bila kubagua na wanasema waonyeshwe bidhaa zipi zinazopaswa na zisizopaswa kulipa ushuru kulingana na makubaliano ya COMESA shirika ambalo nchi hizo zote ni wanachama.

“ tunaleta maharagwe wakatuzuia, unga,sukari na kadhalika na wakatunyakua na kuenda navyo. Walituahidi wataweka orodha ya bidhaa zote ila tumengoja hadi tuchoke” asema Mujawamariya Agnes

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hata hivyo Bw Rwiririza Gashango Kiongozi mratibu wa Ofisi ya Kodi ya Rwanda (RRA) kwenye jimbo la magharibi, alieleza kinagaubaga makubaliano haya.

“Kulikuwa na makubaliano kati ya nchi mbili ambayo hayajakamilika bado, makubalino hayo yanahusu kufutwa kwa ushuru wa forodha kwa bidhaa zisizozidi gharama ya 2000 za dola za Marekani, jopo la watalaam lingali linashughulikia hilo na naamini liko karibu kutimizwa” asema mratibu

Alieleza kwamba makubaliano hayo yayajaanza kutekelezwa kwa sababu kuna yanayopaswa kukosolewa kama cheti ya asili ya bidhaa( certificate of origine). Ingawa bidha hizi hazijabainishwa zile zenye asili ya kilimo na mifugo zinakadiria 170.

Ni desturi ya raia wa Kongo na Wanyarwanda kuwa na uhusiano wa karibu wa kibiashara hususani wale wenye eneo karibu na mpaka ambapo kila upande huvuka kutembeana katika masoko na magulio ya karibu na makazi yao kati ya nchi hizo mbili.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com