kwamamaza 7

Wachambuzi: Jen. Kale Kayihura ni muathiriwa wa ukabila

0

Wachambuzi wa mbambo ya kisiasa nchini Rwanda ama Uganda wanatoa maoni tofauti kuhusu kisa cha Jen. Kale Kayihura. Hata hivyo, jambo moja linalohusisha uchambuzi wao ni suala la ukabila katika uongozi wa Rais Yoweli Museveni.

Hawa wachambuzi wanasema kwamba cahangamoto zilianza kuzuka baada ya Kayihura kupata cheo cha Jenerali na kuwa Kiongozi wa Polisi ya Uganda. Kwa hili, Wengi mwa wafuasi wa kabila la museveni ambalo ni ‘Munyankole- Omuhima’ walianza kujawa na wivu kwa mafanikio ya Kayihura ambaye hana uhusiano wowote na kabila hili.

Wachambuzi wanasema  kwamba anayaoshtakiwa Kayihura hayana uhusiano na mambo ya kuanzisha uhaba wa usalama.

Hali ya suala la Ukabila kwa Bahima

Chombo cha habari Virunga Post kiliandika kuna suala la  wanakabila wa Museveni wenye nguvu zaidi kwenye utawala wa Museveni wakiwemo Luteni Jenerali Henry Tumukunde wanalenga kutawala milele. Kwa hiyo, hawalelewi namna ambavyo Kayihura mwenye asili wilayani Kisoro ambaye si Mnyankole anapanda ngazi kila siku.

Virunga Post iliandika kuwa siyo kufichua siri kusema kwamba Bahima waliwaudhi watu wengine. Hiki chombo cha habari kiliandika

“ Kama kayihura alikuwa anafanya kazi nzuri,mtu kama Henry Tmukunde Muhima mkubwa hawezi kumkubalia kuendelea”

“ Mkuu wa Polisi na Tumukunde wanapambana kuonyesha nani mwenye nguvu” Mbunge Winnie Kiiza alisema.

Habari zilienea kwamba Kayihura alikabiliana na changamoto ambazo hazikumuruhusu kufanya kazi yake vilivyo.

Mchambuzi mwingine alisema kwamba Rais Museveni amepoteza nguvu za kujadili haya masuala ya ukabila na “ Wahima ndio wanyama wakubwa wanatawala mwitu”

Isishaulike kwamba vyombo vya habari nchini Uganda viliandika mala nyingi kuwa Kayihura ni mtu mwenye maadili na kuwa alipendeza raia wengi hadi walipomuita “ macho na masikio ya Museveni”, ‘Museveni’s bule eyed man’ ama mr tear gas kulingana na alivyopambana na suala la maandamano ya wapinzani.

Ikumbukwe kwamba Jen. Kayihura alikamtwa siku tano zilizopita kutoka wilayani Lyantonde na kurejeshwa mjini Kampala ili kuhojiwa.

Kwa sasa amefungwa kwenye kituo cha jeshi cha Makindye,mjini Kampala.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.