kwamamaza 7

Wabunge kutoka Burundi na Tanzania waukosoa ushindi wa Mnyarwanda  kuongoza bunge la Jumuia ya Afrika ya Mashariki

0

Wabunge kutoka Burundi na Tanzania wameukosoa ushindi wa Mnyarwanda Martin Ngoga ambaye amechaguliwa jana mjini Arusha,Tanzania kuongoza bunge la Jumuia wa Afrika Mashariki,EALA kwa kura 33 baadhi ya 36.

Wabunge wa Burundi na Tanzania wametangaza kuwa uchaguzi huu hauwausi na kuwa matokeo yake hayana thamani kwao.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wabunge wa Burundi kwenye jumuia hii kupitia barua yao wamesema kuwa nafasi hii inastahili kuwa ya Burundi na kuwa kinyume na hili ni ukiukaji wa sheria.

Kwa upande mwingine Ofisi ya EALA imetangaza kuwa hakuna ukiukaji wa sheria kwa kuwa lililotokea ni kubadilishana nafasi hii tangu mwaka 2001 kama kawaida.

Wabunge wa Burundi kupitia kiongozi wao,Isabelle Ndahayo amesema kwamba haina budi kueleza waziwazi suala hili la kubadilishana uongozi wa EALA kabla ya kupiga kura ili kujilinda kutoelewana.

Mbunge kutoka nchini Kenya,Peter Matuki ametangazia VOA kuwa nafasi hii inastahili kuwa ya Rwanda kwa kuwa katibu mkuu wa EAC ni raia wa Burundi na kwa hiyo haiwezekani raia wa Burundi mwingine  kuongoza EALA.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Huyu amesema kuwa hili ni kuleta mgogoro ulioko kati ya nchi hizi katika masuala ya eneo la Afrika Mashariki.

Mala nyingi Tanzania na Burundi hupiga marufuku mambo mengi ya Jumuia ya Afrika Mashariki kama vile uhamiaji wa wakazi kutoka nchi shiriki kwenye jumuia hii.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.