Home SIASA Waangalizi wa kura 27 wa EAC miongoni mwa wengine 1200 waliokwisha idhinishwa
SIASA - July 20, 2017

Waangalizi wa kura 27 wa EAC miongoni mwa wengine 1200 waliokwisha idhinishwa

 Waangalizi wa kura wapatao 27 wamekwisha idhinishwa na Jumuiya ya Afrika ya mashariki kwamba watakuja kusimamia uchaguzi mkuu wa Rwanda utakaofanyika mwezi ujao.

Mojawapo wa waangalizi wa uchaguzi ambao wamekwisha asili nchini Rwanda wanasema kwamba wamefurahia hali ya utulivu iliyoko nchini Rwanda wakati huu Rwanda inapojiandaa kumchagua Rais katika Uchaguzi wa mwezi ujao kama alivyosema Charles JK Njoroge mmoja wa waangalizi hao na akiwa ndiye mkuu wa waangalizi hao.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waangalizi hawa baada ya kuasili Rwanda walizungumza na maafisa wa Tume ya Uchaguzi na kuelezewa kuhusu mpango wote wa uchaguzi.

Njoroge aliusifu mpango wa uchaguzi kwa kusema “Nimekuwa hapa kwenye uchaguzi uliopita na kwa kurudi hapa naona hali iko tulivu na hilo ni jambo la muhimu kuiga. Kumekuwa na wakati nchi nyingine zikakumbana na ghasia za kuufuata uchaguzi lakini hapa naweza nikasema kwamba inafaa kuwa wananchi wanachagua kwa usalama, wakamchagua ambaye wanamtaka, na anayeshindwa akajua ni hivyo tu kwamba kutakuja wakati mwingine na wakajaribu bahati yao”.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi naye alifurahia kuwapokea waangalizi hawa kwa kusema inaashiria kwamba mambo ya Tume yanaenda sawa na inafanya kazi kwa haki.

Hakuna waangalizi wa kura wanyarwanda waliopelekwa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuangalia shughuli za kura hii. Na ndivyo hali ilivyo kwa upande wa uchaguzi utakaofanyika nchini Kenya hakutakuweko na waangalizi wa kura wakenya ila waangalizi kutoka Rwanda watakwenda kuangalia uchaguzi wa kura Kenya na Wakenya kuja kuuangalia wa Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.