kwamamaza 7

Waakilishi wa Burundi katika EALA wanakanusha kushiki mkutano utakao fanyika Kigali

0

Wabunge 5 kati ya 9 waakilishi wa Burundi katika bunge la jumuia ya Afrika Mashariki EALA hawatashiriki mkutano unao tarajiwa kufanyika Kigali kwa sababu ya hewa mbaya kati ya nchi yao na Rwanda.

Mkutano huo wa tano unatarajiwa kufanyika Kigali tarehe 5 hadi 17 Mach 2017, ila wabunge 5 wa Burundi wameandikia uongozi wa EALA nia yao ya kutoshiriki mkutano.

Tarehe 18 Januari ndipo kiongozi wa EALA, Daniel Kidega aliongea na hao wabunge kuhusu swali hilo na ndipo wakasema ya kuwa hawatashiriki kwa hali ya siasa kati hizo nchi mbili nimbaya kama vile husema The East African.

Katika barua walio andikia mbunge Kidega walisema ya kuwa uhusiano kati ya Burundi na Rwanda si mwema kwa hio hawatashiki mkutano unao tarajiwa fanyika Kigali mwezi Mach.

Wakati gaziti la The African lilijaribu kuzungumza na mbunge Kidega, kiongozi wa EALA hakutangaza mengi kuhusu swala hilo, ila taarifa kutoka EALA husema kwamba wabunge wote kutoka Burundi hawakukataa kushiriki huo mkutano.

Hii kukataa kushiriki mkutano kwa wabunge wa Burundu ni alama inayo onyesha ya kuwa hali ya uhusiano kati nchi jirani unaendelea kuwa mbaya baada ya mzozo ulio anza tangu mwaka wa 2015, Burundi ikishutumu Rwanda kuwasaidia wapinzani wa rais Nkurunziza.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.