Neno shetani ni maarufu katika vitabu vya dini na katika mazungumzo. Hata hivyo, kuna mambo kadhaa ambayo bado yana utata

  1. Ufiche wa Shamba la Edeni

Imesemekana kuwa nyoka aliyemshawishi Hawa kula tunda lililokuwa limekatazwa alikuwa ni Shetani. Hii ni licha ya kuwa hakuna andiko linalotaja Shetani moja kwa moja.

Aidha, wasomi wa Biblia wamejadli wakisema kuwa kuwepo kwa Shetani hakukuwa kumehakikiwa wakati wa kuandikwa kwa kitabu cha Mwanzo katika Biblia.

Kwa hiyo iwapo nyoka si shetani, ni nini?

  1. Ufiche wa hesabu ya watu iliyofanywa na Daudi

Katika kitabu cha Samuel (2 Samuel 24), Mungu anakasirishwa na Israeli na hivyo kumchochea mfalme Daudi kutekeleza shughuli ya kuhesabu watu, na kisha kuwaadhibu kwa maafa.

Katika kitambu cha kwanza cha Mambo ya Nyakati mlango wa 21, inasemekana ni shetani aliyemtaka Daudi kufanya hesabu hii.

Ni Mungu au Shetani aliyemwelekeza Daudi kufanya hesabu hiyo?

  1. Ufiche wa jina

Je, Shetani ana jina? Neno “Shetani” linamaanisha adui au mshitaki katika lugha ya Kiyahudi.

Katika Agano la Kale la Biblia, neno hilo linatumika kwa wanadamu.

Kwa mfano, mfalme Rezon wa Syria anasemekana kuwa Shetani (adui) wa Suleiman.

Je, shetani alikuwa na jina?

  1. Ufiche ya kuzimu

Inaaminika kuwa Shetani ndiye anayetawala kuzimu anakowatesa waovu. Hata hivyo, kauli hii haiko kwa Biblia.

  1. Ufiche wa Shetani katika Agano la Kale na Agano Jipya

Shetani anajotikeza katika matukio mawili katika Agano la Kale.

Kwa wakati mmoja, Shetani yuko mbele za Mungu akimshitaki Ayubu na kumtaka Mungu kumpa ruhusa ya kumtesa Ayubu.

Aidha, tukio lingine ni katika kitabu cha Zakaria ambako kuhani Yoshua anasimama mbele ya mahakama ya mbinguni. Shetani anamshitaki Yoshua lakini malaika wa Mungu anamtetea.

Katika matukio hayo mawili, Shetani anajitokeza kama anayemtumikia Mungu kama mshitaki mkuu.

Kwa upande mwingine, katika Agano Jipya, Shetani anatajwa kama “mkuu wa mapepo” na aliyejaa uovu.

  1. Ufiche wa nguvu za shetani juu ya dunia

Katika Agano la Kale, Shetani anayaharibu Maisha ya Ayubu mara moja baada ya Mungu kumpa ruhusa.

Katika Agano Jipya, Shetani anamjaribu Yesu kutumia nguvu zake. Kwa mfano, anapohisi njaa, Shetani anamwambia Yesu kubadilisha mawe kuwa mikate.

Je, Shetani ana nguvu ulimwenguni?

  1. Ufiche wa sura ya Shetani

Kuna watu walio na picha ya Shetani (pembe za mbuzi, miguu na akiwa amebeba uma kubwa). Hata hivyo, maelezo haya hayako katika Biblia.

Taswira hii ilitoka wapi?

  1. Ufiche wa Shetani katika Uislamu

Waislamu wanaamini kuweko kwa Shaytan (Shetani) ambaye pia anaitwa Iblis. Katika Koran, Shetani alikataa kumsujudia Adamu akisema, “ Mimi ni bora kumliko; uliniumba kutokana na moto nay eye kutokana na tope”

Licha ya kukasirishwa na tendo hilo, Allah anachelea adhabu huku Shetani akijaribu kuonyesha ukweli wa maneno yake kwa kuwajaribu wanadamu kufanya dhambi.

Kwa upande mwingine, Koran inasema kuwa Allah aliwaamrisha malaika wote akiwemo Iblis kumsujudia. Hii ni kumaanisha kuwa Shetani ni malaika.

  1. Je, Shetani katika Koran alikuwa amekosa?

Kuna wasomi na wafuasi wa Wasufi ambao wamedai kuwa Shetani hakukosea kwa kukataa kumsujudia Adamu kwani malaika hawastahili kusujudia mwingine ispokuwa Mungu.

Hata hivyo, maoni haya hayakubaliwi na Waislamu wa madhehebu mengine.

  1. Ufiche wa Shetani na Mpinga Kristo

Katika Agano Jipya, kuna vifungu vinavyotaja kuja kwa Masihi wa uongo au Mpinga Kristo. Ingawa Mpinga Kristo anahusishwa na Shetani, Biblia imetaja kuwa wawili hao hawahusiani.

Kwa hiyo kuna uhusiano gani kati ya Shetani na Mpinga Kristo?

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.