Viongozi wawili wa wilaya ya Kayonza wametiwa mabaroni baada ya upelelezi ulio fanywa kwa ajili ya walimu walio pewa kazi katika wilaya hio.

Bizimana Francois Xavier, kiongozi wa malezi katika wilaya pamoja na Mugabo Namara Charles anaye husika na sekondari na elimu ya msingi katika wilaya walitiwa mbaroni juma tatu baada ya kushitakiwa na walio fanya mtihani wakisema ya kuwa majina yao hayakuonekana kwenya orodha yenye ilitumiwa wahusika wa elimu REB ijapo kuwa walishinda kwenye mtihani wa nyuma wa kusema. Kupitia ombi la REB polisi ilianza upelelezi kwa ajili ya swala hilo.

Msemaji wa polisi jimbo la Mashariki, Inspector of Police (IP) Emmanuel Kayigi, alisema ya kuwa watu hao wawili walibadilisha alama na kuongezea wale ambao walishindwa.

IP Kayigi eti: « wilaya ilipana kazi kwa walimu 62, kawaida wanao husika na mtihani husahihisha hapo kwenye mitihani kafanyika baada ya hapo ripoti ya walio shinda ao kushindwa hupewa viongozi hao wawili ».

Ilionekana ya kuwa alama wahusika na kukosoa wazilizo wapo hao viongozi wawili ni tofauti na alama ambazo zilipewa REB, pia upelelezi ulionyesha ya kuwa vikaratasi vya watu 32 walio shindwa mtihani wa kusema vilitiwa katika wale ambao walishinda.

Upelelezi ulionyesha ya kuwa kuna mtu ambaye alikuwa amepata alama 6 kisha mbele ya wakaweka 9 na ikageuka 96 kwa mia namwengine alikuwa na 33 ikabadilishwa kuwa 93.

Ili wale ambao walishindwa watiwe kwenye orodha ya washindaji walikuwa wakiombwa pesa ya Rwanda kati ya 200.000 na 300.000.

Kwa kumalizia alisema ya kuwa hakuna atakaye vumilia rushwa Rwanda, kuipiganisha ni moja ambayo Rwanda inatilia mkazo tena raia sherti wasonge mbele katika ngazi zote bila kujali atakaye husika na rushwa na akitoa uito kumushota kidole.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.