kwamamaza 7

Viongozi waitwa kukuza huduma kwa wananchi

0

Rais Paul Kagame ambaye ni kiongozi  mkuu wa chama cha RPF Inkotanyi kinachoongoza aliwaita viongozi kukuza huduma kwa wananchi na kuweka mbele maslahi ya wananchi kwani ni majukumu ya viongozi kuwahudumia raia.

Mwito ulitolewa jana katika mkutano wa Chama cha uongozi cha RPF Inkotanyi, mkutano ambao ulishirikiwa na viongozi washiriki wa Chama cha siasa, mashirika binafsi na wananchi wanaoishi nje takribani 2000.

[ad id=”72″]

“Hakuna kiongozi hapa anayeweza kuwa muhimu kuliko nchi wanayohudumia. Kuna viongozi wanaolevywa na kujisifu wakaanza kufikiri kwamba maslahi yao binafsi yanakuwa juu ya yale ya nchi.” Kagame alisema.

31455506021_ce6f7878a0_z

Kuhusu huwahudumia wananchi, viongozi hawa walikumbushwa majukumu. “Kuwahudumia vizuri raia si fadhila lakini ni majukumu ya viongozi.” Mwenyewe kagame aliongeza.

Kagame aliwakumbusha waliotoa mwili wao kama kafala ya kuikomboa nchi mikononi mwa viongozi wabaya waliosababisha mauaji ya kimbari.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.