kwamamaza 7

Viongozi wa viwango wahamasishwa kukuza kanuni za uongozi

0

Wakati wa kufunga masomo ya viongozi wa viwango katika taasisi za serikali, waziri mkuu wa Rwanda; Mheshimiwa Anastase Murekezi amewambia viongozi hawa kukuza kanuni za uongozi na kutia kwa vitendo masomo waliosoma kwa muda wa siku kumi.

Sherehe za kufunga masomo ya uraia kwa waliopewa jina la ‘IMBAMBURIRAMIHIGO’; zimefanyiwa leo 27 Novemba 2016 katika kiwanja cha Kamena, wilayani Huye.

15227937_1233481040043908_1235465519_n

Miongoni mwa ahadi zimetolewa na viongozi hawa, wamewahidi kutokosa majukumu na kufuatilia miradi ya serikali ya kukuza maendeleo, kuwahudumia vizuri raia na kulinda mafanikio ya nchi.

“Baada ya kumaliza masomo muhimu ya uraia, tunatarajia mengi kutoka kwenu na kazi nyingi kali zinawasubiri. Tunawatarajia nyinyi kuwa viongozi wema na kuwa nguzo ya mipango ya kisiasa ya serikali ili kutekeleza miradi mbali mbali ya mabadiliko mazuri na ustawi wa kuelekea katika maono ya 2020 na pia ya 2050.” Waziri mkuu Murekezi alisema.

Waziri mkuu
Waziri mkuu Anastase Murekezi, waziri wa utumishi wa na kazi Bi Uwizeye Judith na viongoozi wanafunzi

Waziri wa utumishi wa umma na kazi, Judith Uwizeye ambaye alihudhuria sherehe, ametoa wito kwa viongozi hawa wa kuwa na sifa ya sharti binafsi ya kufanya kazi na kutimiza majukumu kwani hiari yashinda utumwa.

[ad id=”72″]

“Upendo wa kazi na heshima huhitajika ili kutimiza vizuri majukumu. Kuna mambo mengi mmesomea hapa, kinachobaki ni kurejea kwenye maeneo yetu ya kazi na kutekeleza tulioyasoma pamoja na kuongozwa na masomo tumepata tangu tulipofika hapa.” Waziri Uwizeye amesema.

Serikali imeanzisha masomo haya ya uraia anayejulikana kienyeji kama ‘Itorero’ kwa niaba ya kuhamasisha ufahari mwema miongoni mwa wanyarwanda na kukuza utashi wa kujitolea. Takwimu huonyesha kwamba raia 243, 284 wamehudhuria masomo haya tangu 2007 hadi 2012.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.