kwamamaza 7

Viongozi wa Rwanda walaani madai ya mgombea wa urais nchini Zimbabwe

0

Rais Kagame na viongozi wengine wamekanusha madai ya mgombea wa urais nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa aliyesema kuwa alimshauri Rais Kagame namna ya kujenga Rwanda hususani mambo ya teknolojia.

Rais Kagame ameeleza hamjui Nelson Chamisa na kuwa hawakukutana popote.

“Cha kwanza jina langu si Kagama ni Kagame, cha pili sijui huyu mwanamumwe sikuzungumza naye, cha tatu ni kwamba siasa ya teknolojia ya Rwanda na miradi yake ilianza kabla ya uwepo wa MDC na siasa zake,nawatakia mema raia wa Zimbabwe”

Waziri wa Mambo ya Nje,Ushirikiano na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Louise Mushikiwabo ameeleza hajui kama huyu Nelson Chamisa alikutana na Rais Kagame.

Pia, Afisa kwa Mawasiliano ikuluni maarufu kama Village Urugwiro,Yolande Makolo amesema kuwa Chamisa anadanganya kwa kuwa anayosema hayakutokea.

“Anadanganya, sikumsikia. Hana lolote la kufanya kuhusu uchumi wetu”

Pengine, Nelson Chamisa jumamosi alipokuwa eneo la Betbridge alisema kwamba alimshauri Kagame namna ya kuboresha uchumi kupitia teknolojia.

Alisema” Angalia anavyofanya ndugu yangu Rais Kagame,nilimsaidia kuhusu siasa yake ya tekonolojia tulipokutana mjini Geneva,Switzerland.Alifurahishwa na ushauri wangu”

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.