kwamamaza 7

Viongozi wa Burundi wahusishwa katika mpango wa kushambulia Rwanda kwa kumsaidia Jen. Kayumba

0

Kuna taarifa ambazo chombo cha habari kinahakikisha  ni aminifu kwamba baadhi ya viongozi nchini Burundi kuna wanaounga mkono mipango ya kushambulia Rwanda kwa kusaidia shuguli za chama cha upinzani kwa Rwanda (RNC) cha Jen. Kayumba Nyamwasa.

Kwa mujibu wa chombo cha habari The Great Lakes watchman hawa viongozi ni  Katibu Mkuu wa chama tawala nchini humo (CNDD-FDD),  Jen. Evariste Ndayishimiye.

Katibu Mkuu wa CNDD-FDD Jen. Evariste Ndayishimiye

Huyu aliahidi kusaidia mipango ya RNC kwenye mkutano na mwanasheria wa hiki chama nchini Uganda, Edgar Tabaro Muvunyi wiki iliyopita.

Pia Ndayishimiye alihakikisha kutakuwepo ushirikiano na RNC na kuwa ana mpango wa kumkuta Jen. Kayumba kwa kutimiza ilivyoahidi serikali yake.

Pia Tabaro alikutana na Jen. Steve Ntakarutimana ambaye alimuambia serikali ya Burundi itatoa msaada zaidi baada ya RNC kuwa na mahali pengine pa kutoa uwezo wa kuezesha mpango wake.

Jen. Steven Ntakarutimana

Mwingine ni  Mshauri wa mambo ya usalama wa Rais Nkurunziza, Jen. Agricole Ntirampeba, Jen. Emmanuel Sinzohagera na mfanyabiashara bingwa, Thomas Ndacyayisenga.

Hizi taarifa zinaendelea kusema mkutano huu na viongozi wa Burundi ni ishara ya  kuwa kuna  ushirikiano kati ya maafisa wa usalama nchini Uganda na Burundi kuisaidia RNC.

Hizi taarifa ni baada ya  Virunga Post miezi iliyopita kutangaza Mkuu wa Jeshi nchini Burundi  Jen. Prime Niyongabo anashiriki katika vitendo vya kusajili wanajeshi wa RNC.

Hiki chombo cha habari kilikuwa kikisema wanaosajiliwa wanatoka nchini Uganda na kupita nchini Burundi kisha wakasindikizwa na jeshi la Burundi  kuenda kwenye kambi za jeshi la Kayumba Nyamwasa eneo la Minembwe nchini DR Congo.

Hata hivyo, RNC ililaani kuna kambi za jeshi lake nchini  DR Congo.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.