kwamamaza 7

Viongozi 19 wa Viini wameacha kazi ya serikali

0

Katika wilaya ya Nyamasheke, viongozi 19 wa viini wameacha kazi ya serikali bila kusukumwa jana tarehe 11 Januari 2017.

Kamali Aime Fabien, kiongozi wa wilaya hio amesema kua walio acha kazi ni katika kata 11 kati ya kata 15 ambazo huunda wilaya ya Nyamasheke, wakiwa wanawake 2 na wabwana 17.

Viongozi hao walikua wamekuja katika mkutano wa usalama wa wilaya, kwa punde kidogo viongozi wa mkutano wakaomba watangazaji habari kutoka inje, muda kidogo ndipo wakatangaza kuwa wameacha kazi kwa niaba yao.

Meya Kamali amesema kuacha kazi kwao haitatia tatizo kwa kuwa watafanya haraka ili kutia wengine viongozi.

Ameomba wakaaji kutokuwa na woga akisema ni kawaida kama mtu anazofika sherti aache kwani nchi yetu ni haraka kwa maendeleo.

Hao 19 wamefuatana na wengine 5 wa kata katika wilaya hio ya Nyamasheke walio acha kazi siku zilizo pita na mpaka sasa nafasi zao bado kuchukuliwa.

Na katika wilaya ya Rusizi wengine viongozi wa viini 26 waliacha kazi zao jana na hizo wilaya zote ni katika jimbo la Mangaribi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.