kwamamaza 7

Vijana wa RPF waapa kupambana na ugaidi

0

Vijana wa wilaya ya Rubavu kutoka katika chama cha RPF Inkotanyi kinachoongoza nchini Rwanda wameapa kupambana na vitendo vya ugaidi na biashara ya binadamu ili kulinda wananchi. Waliapa katika mkutano wa vijana wa RPF ulipatiakana tarehe 15 Oktoba 2016.

Kiongozi wa vijana wa RPF wilayani Rubavu, Jean Bosco Tuyishime alisema kwamba mkutano wa familia ya RPF Inkotanyi umewafaidikisha mengi zaidi kuhusu kufanyia nchi yao.

“Tumepata maonyo zaidi kuhusu kupambana na biashara ya binadamu na ugaidi pamoja na dawa za kulevya. Sisi vijana, nguvu za taifa; tutashinda mapambano hayo kwa kupitia kwa mazungumzo na vijana wengine katika wilaya”.

[ad id=”72″]

Kambabazi Nelson ambaye ni kiongozi wa RPF katika wilaya ya Rubavu alisifu hawa vijana na kuwahamasisha kufanya zaidi ili kuwavutia washiriki wengine.

Alisema kwamba katika mwaka wa 2015-2016 wamefikia lengo kwa kiwango cha 93 %. “Tunawashukuru kwa bidii waliotumia katika vitendo viavyowavutia washiriki”.

Chama cha RPF Inkotanyi kiliundwa na wananchi wa Rwanda. Rais paul Kagame, leti Fred Gisa Rwigema na mashabiki wengine wa Amani na washabiki wa demokrasia walijiweka pamoja na kujeuza chama cha RANU kuwa RPF tarehe 25 Desemba 1987.

Theogene u @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.