Swahili
HABARI SIASA

Vifaa vya kura vyaasilishwa karibu kote : wakazi wa Diaspora wanatarajia uchaguzi kwa hamu

Ikiwa Tume ya Uchaguzi ya Rwanda(NEC) inatangaza kwamba karibu vifaa vyote vya kupigia kura vimekwisha asilishwa kwa vituo vyote vya kupia kura vya nje ya nchi wanyarwanda wa dispora nao wanangojea siku ya kura kwa shangwe.

Kulingana na takwimu za NEC, Wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi wapatao 40.000 ndio wanaotarajiwa kupiga kura Kati ya wagombea watatu ambao ni Frank Habineza wa chama cha Green, Mpayimana Phillipe mgombea huru na Paul Kagame wa chama cha RPF Inkotanyi.

Charles Munyaneza, katibu mtendaji wa NEC amesema kwamba vifaa vya kupigia kura vimekwisha pelekwa kwa bolozi za Rwanda mnamo siku ya Ijumaa na Jumapili kulingana na taarifa ya The New Times.

“tunachokifanya kwa sasa ni kushirikiana na kikosi cha wizara ya mambo ya nje ya nchi kutusaidia kufuatilia ikiwa vifaa hivyo vinawasili kwa maeneo yake.

 Vifaa ambavyo vinatumwa ni pamoja na karatasi za kupigia kura na hata wino na katibu huyo amesema visanduku kulingana na ukubwa wake vimelazimika kununuliwa na balozi za nchi hizo.

Hata hivyo kuna pingamizi kwa wapiga kura hasahasa wa Uchina kulingana na Ukubwa wake na kuweko kwa kituo kimoja cha uchaguzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alex Ntwali ambaye ni mkuu wa muungano wa wanyarwanda wanaoishi diaspora amehakikisha wakazi wa diaspora wako tayari kushiriki kura kwa wingi kwa kuwa wamehamasishwa licha ya kuwa kuna pingamizi ya safari ndefu wanayopaswa kufanya kufikia kituo cha kura kilicho mjini Beijing kwenye makao ya Balozi.

Licha ya pingamizi kama hizo kuna nchi zisizo na matatizo kama haya ambapo wapiga kura hawatalazimika kwenda safari ndefu wakitaka kuvifikia vituo vya uchaguzi.

Nchi hizo ni kama India ambako kumeamriwa kupeleka vifaa vya kura kwenye Vyuo mbalimbali vya nchi humo vitakavyotumika kama vituo vya kura.

Na pia nchini Kanada nako kulisambazwa vituo vine huku Umarekani kukiwa na vituo vya kura kwenye miji tisa mikubwa ya nchi hiyo.

Wakazi wa diaspora watapiga kura tarehe 3 Agosti na Uchaguzi wa ndani ya nchi baadaye tarehe 4 Agosti.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com