kwamamaza 7

Vénusté aomboleza marehemu Mhe. Patrick Mazimpaka

0

Aliyekuwa fisa wa mawasiliano wa UNAMIR, Bw Venuste Nshimiyimana, ameomboleza Mhe. Patrick Mazimpaka,mwanamume anayemuona kuwa shujaa kwa Rwanda na Afrika kwa ujumla.

Akieleza alivyomuona, Nshimiyimana amesema kuwa alimkuta marehemu mala ya mwisho mwaka 2014 mjini Hague walipokuwa kwenye mkutano na kuwa alikuwa mtu mwenye busara na hesehima ya kibinadamu.

Nshimiyimana ameeleza”Nimekuja hapa leo kumpa heshima mmoja mwa wahunzi wa mkataba wa Arusha,Patrick Mazimpaka alikuwa kimaumbile mwanadiplomasia (…)”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Alikuwa makamu mwenyekiti wa chama cha RPF lakini alikuwa mpole na kumheshimu yeyote”ameongeza.

Pengine,Bw Venuste Nshimiyimana amezungumzia walivyomuona wengine kwenye mkutano mnamo mwaka 1993 eneo la Ngondole kama wale Meja Jenerali  Egundayo Babakayode Opaleye aliyekuwa akimuita “Wise man”yaani mhenga.

Ameongeza kuwa marehemu Mhe. Patrick Mazimpaka alikuwa  mtu wa kuaminiwa, ila hakuweza kuhudhuria siku ya msiba wake kama alivyofanya kwa marehemu Kayitare Intare Batinya ambaye chanzo cha kifo chake hakiuleweka waziwazi.

“Nitaambia dunia nzima kwamba na Wanyarwanda kwamba ulipambania uhuru na umoja wao na kugawana vilivyo mali yote miliki ya nchi” Venuste ameahidi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Ulitimiza wajibu wako vilivyo ulipokuwa madaraka ya makamu  mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika,ulikuwa adili kwa nchi yako na kwa mola,Imana”Bw Nshimiyimana amenena

Patrick Mazimpaka aliaga dunia tarehe 25 Januari nchini Uhindi akiwa na umri wa miaka 69.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.