Kifo cha mfalme wa mwisho wa Rwanda kimetoa utata na kutokubliana kuhusu mahali pa kuzika maiti yake, Kigeli V Ndahindurwa. Washiriki wa familia yake  wanaoishi nchini Rwanda wanataka mazishi yake kufanyiwa katika nchi ya kizazi na wengine wachache wanaokuwa Marekani wanahitaji mazishi kufanyiwa Marekani.

Katika mkutano kati ya wandishi wa habari na familia ya mfalme mnamo tarehe 21 Oktoba 2016, washiriki wa familia ya mfalme wanaoishi nchini Rwanda walikubaliana mazishi yake kufanyiwa Rwanda.

Mahitaji ya wanafamilia wa Rwanda, hayakukubaliwa na wenzao wa Marekani. Jumatano, kundi la watu tisa wakiwemo wanafamilia na Ezra Mpyisi aliyekuwa mhudumu wa mfalme; walifika Marekani kwa kuzungumza kibinafsi na wanafamilia wanaoishi Marekani.

[ad id=”72″]

Mpyisi alisema kuwa wana matumaini kwamba wanafamilia wa Marekani watakubali mazishi ya mfalme kufanyiwa nchini Rwanda. Aliongeza kwamba kama hawatakubaliana, itakuwa lazima kuomba msaada serikali ya Marekani katika uamzi.

Alisema, “Tunakuwa na matumaini ya kutosha ijapokuwa hatujafika kwenye suruhisho ya mwisho bado, tungali mazungumzoni nao.”

[ad id=”72″]

Wanafamilia wa mfalme hawajasema kama Kigeli V Ndahindurwa aliamua kuhusu mahali pa kuzikwa kabla ya kifo chake. Mhudumu Mpyisi alisema kwamba kama alisema kuhusu mazishi yake wataongea na walikokuwa na mfalme kuhusu jambo hilo.

Mfalme Kigeli V Ndahindurwa alifariki usikuni Jumamosi mnamo tarehe 16 Oktoba 2016. Alikuwa na umri wa miaka 80, na alifariki angali kapera kwani alisema kuwa mfalme hawezi kuoa akiwa uhamishoni.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.