Muimbaji Joseph Mayanja maarufu kama Dr.Jose Chameleone amemuonya nduguye Douglas Mayanja maarufu kama Weasel kutotegemea tajiri Brian Kirumira maarufu kama Brian White anayelenga kujulikana tu.

Tajiri Brian Kirumira aka Brian White(kushoto) na muimbaji Weasel/picha na ugblizz

Haya ni baada ya huyu tajiri mwenye umri mdogo kuweka wazi kwamba atadhamini tamasha zote za Weasel nchini Uganda.

Chameleone ameeleza hili juu ya wasiwasi zake kuwa msaada wa huyu tajiri unaweza kuja ukaharibu kipaji cha nduguye.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Siyo Chameleone tu kumuonya Weasel kuachana na Brian White,taarifa za Ugblizz zimeelza kwamba hata na waimbaji wengine gwiji mwa Afrika Mashariki wamemshauri Weasel kuacha haya baali atie mkazo kwenye kipaji chake cha kuimba.

Baada ya hili Weasel Manizo amekuenda punde si punde kunasa sauti za wimbo wake huko ‘Studio’Makindye.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina