kwamamaza 7

USA yamchukulia hatua Gen.François Olenga, Mkuu wa kikosi cha kumlinda Rais Kabila

0

Marekani yamwongeza kwenye orodha nyeusi Gen François Olenga, Mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa kumlinda rais Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Gen François Olenga, kwa sasa haruhusiwi kukanyaga mguu wake kwenye ardhi ya Marekani , ikimushtumu kutenda dhidi ya Kidemokrasia, kuonea kwa kuwakamata na kuwafunga wanasiasa wa upinzani ili Rais Kabila aendelee kushika madaraka.

Kwa mujibu wa rediyo Okapi, mwanajeshi huyu harusiwi kamwe kuendesha shughuli zake za kibiashara Marekani wala ushirikiano wa namna yoyote wa kibiashara na wamarekani.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine ,mwishoni mwa mwezi Disemba 2016, viongozi wapatao 6 walichukuliwa hatua na Ubelgiji pamoja na Umarekani kwa tuhuma za kuwaoonea wananchi.

Aidha mwishoni mwa mwezi uliyopita halmashauri ya mawaziri wa wa mambo ya nje kutoka nchi za Umoja wa Ulaya iliwachukulia pia hatua nyingine viongozi wa Kongo akiwemo waziri Habari , Bernard Mende, wakashauriwa kuzingatia haki na uhuru wa binadamu

Miongoni mwa viongozi hao walikuwemo pia wanajeshi maafisa wakuu na hata waziri Lambert Mende, wakituhumiwa wote kutochukulia hatua uonevu wanaotendewa wananchi, na hatua hizo dhidi ya viongozi zikachukuliwa kwa sababu ya kesi iliyotokea katikati ya jimbo Kasai.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy/bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.