Swahili
Home » Urusi:Burundi kununua bunduki ya kudungua ndege baada ya kudai ya Rwanda ilionekana katika anga lake
HABARI MPYA

Urusi:Burundi kununua bunduki ya kudungua ndege baada ya kudai ya Rwanda ilionekana katika anga lake

Bunduki ya aina ya Pantsir-S1

Taarifa kutoka nchini Burundi na Urusi zimehakikisha kuna mpango wa kununua bunduki ya aina ya Pantsir-S1 ya kudungua ndege.

Hili ni baada ya viongozi kufunguka ndege ya Rwanda ilionekana katika anga lake tarehe 13 Julai mwaka huu mkoa wa Kayanza kama ilivyohakikishwa na Gavana wake, Anicet  Ndayizeye. miezi iliyopita.

“Nataka kuwajulisha kwamba ndege ya Rwanda ilionekana katika anga letu huku wilayani Kabarore. Ilikuja na kuchunguza vituo vyetu vya jeshi na kurudi nyuma” Gavana Ndayizeye alisema

Waziri wa Ulinzi, Emmanuel Ntahomvukiye

Taarifa za Russian TV kutoka Ofisi ya Utangazaji nchini Urusi (RIA Novosti) zimekamilisha kuna mpango wa kununua hii silaha ya kujikinga uvamizi wa angani.

Pia hizi taarifa zilihakikishwa na Waziri wa Ulinzi nchini Burundi, Emmanuel Ntahomvukiye alipokuwa kwenye mazungumzo na  watangazaji tarehe 24 Ogasti mwaka huu nchini Urusi.

“ Ina nguvu, nchi yangu inataka kuinunua”

Waziri Ntahomvukiye alieleza haya baada ya Urusi kutia saini kwenye mkataba wa ushirikiano wa kijeshi.

Pantsir-S1 ina bei ya miliyoni $ kati ya 13.15 na 14.67. na inabebwa na gari linaloiwezesha kusafirishwa.

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com