Swahili
HABARI MPYA

Urafiki wa dhati kati ya tajiri Rujugiro na serikali ya Rais Nkurunziza watiwa hadharani

Handmade Software, Inc. Image Alchemy v1.14

Taarifa zimezagaa kwamba kuna urafiki wa dhati kati ya tajiri Ayabatwa Tribert Rujugiro,76, na viongozi wa serikali ya Burundi, jambo ambalo linamuwezesha  Rujugiro kuendelea na shughuli zake za vitendo vya kuudhi serikali ya Rwanda.

Taarifa za chombo cha habari nchini Kenya,The Standard zinasema kuwa urafiki  huu uliwezekana kutokana na  kuwa tajiri Rujugiro anawapatia zawadi za bure viongozi wa Burundi kama vile  hisa katika kampuni zake za sigara na simenti.

Pia, tajiri Rujugiro alihakikisha urafiki huu miaka miwili iliyopita alipodhamini chama tawala nchini Burundi,CNDD-FDD katika kampeni za uchaguzi wa rais.Tajiri Rujugiro alitoa fedha ambazo hazikutajwa kiasi pamoja na magari 40 mapya ya kurahisisha usafirishaji wakati wa kampeni za CNDD-FDD.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine, taarifa hizi zimeeleza kuwa si mala ya kuanza mzee tajiri Rujugiro  kuwa rafiki wa mmoja mwa marais wa Burundi kwani alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Jean Baptiste Bagaza tangu mwaka 1970 hadi 1980.

Haya ni baada ya Virunga Post kutangaza kuwa mkuu wa jeshi la Burundi,Jenerali Prime Niyongabo anasaidia chama cha RNC kusajili wanajeshi na kuwasindikiza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo eneo la Minembwe.

Kuna taarifa kwamba mzee tajiri Rujugiro ni mdhamini wa chama hiki cha upinzani kwa serikali ya Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com