kwamamaza 7

UPDF wamepeleka jeshi kubwa mpakani na DRC ikisema M23 kwenye mapambano

0

Jeshi la Uganda pamoja na vifaa vya vita wamekwenda kulinda mpaka wao na nchi ya Congo karibu na mji wa Bunagana, wilaya ya Kisoro kwani husemwa kuwa kumeonekana silaha nyingi na kua M23 imezua mapambano.

Silaha 6 za aina ya machine gun, aina ya PK machine gun, na masasu vimekamatwa na polisi vikipakizwa ndani ya gari ya aina ya “Premio” yenye namba UAS 978B.

Watu hao walio kamatwa hawakujulikana ila walikimbia na kuingia msituni Congo walipo ona kua polisi ya Ugana imewagundua.

Kiongozi wa Kisoro, Hajji Shafique Ssekandi, amesema kua wanajeshi wa Uganda wamekwenda kulinda usalama mpakani wakati upelelezi ukiendelea kufanywa kwa ajili la tatizo hilo.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Miaka 3 nenda, kundi la M23 walio piganisha serikali ya Congo, walifanya mapigano makali hapo sehemu ya mpaka wa Bunagana na mabomu ziliangua Uganda hata Rwanda na watu walijeruhiwa, na wakimbizi wengi kakimbilia Uganda.

Taarifa hii huja ikifuatana na nyingine ambayo ilikua ikisema kuwa wapiganaji wa M23 wamevuka mpaka wakitoka ukimbizini.

Musemaji wa serikali ya Congo, Lambert Mende, amesema kuwa karibu wapiganaji 200 wa M23 wameingia wakitoka Uganda na kuteka kijiji katika kivu ya Kasikazini kama vile husema AFP.

Aendelea na kusema ku jeshi la Congo (FARDC) walipambana na vikosi 2 sehemu ya Ishasha, ijapo kua wangelikua Uganda wakichunguzwa na uongozi wa Uganda.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo husema kua kikosi kimoja kilikuwa kikiongozwa na Gen Sultan Makenga.

Hata kama serikali ya Congo yahakikisha hayo, waziri wa mataifa wa Uganda yeye hukana kuwasaidia M23 kuvuka mpaka, hayo akizungumza na AFP mjini Kampala.

Waziri Oryem aendelea na kuomba serikali ya Congo kutafuta suluhisho la tatizo lao bila kutaja Uganda.

Kiongozi wa polisi hapo Kisoro amesema kua silaha zilikamatwa zimepelekwa kwenye kikako cha polisi hapo Kisoro.

Abel Bizimana, kiongozi wa wilaya ya Kisoro hizo silaha ambazo zimekamatwa huonyesha usalama kidogo katika wilaya hio.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.