kwamamaza 7

UNHCR yatangaza kuwarejesha takriban wakimbizi elfu 175 wa wanyarwanda

0

Kwa mjibu wa Rwanda News Agency, UNHCR (Shirika la Umoja wa Mataifa idara ya wakimbizi) imetangaza kwamba iliwasaidia kurejea nchini Rwanda takriban ya wakimbizi elfu mia moja sabini na tano(175,000) kutoka mwaka wa 2000.

“hadi sasa tumewahi kuwarejesha nchini Rwanda wakimbizi 3000 kutoka mwanzo wa mwaka huu, na tumewarejesha jumla ya wakimbizi elfu 175 kutoka mwaka wa 2000” mfanyakazi mmoja katika UNHCR asema.

Idara hii ya wakimbizi ya UN inaendelea kuwasaidia Wanyarwanda wanaotaka kurejea, ambako iliweka Ofisi mbalimbali za kuwapokea katika mji wa Goma na Bukavu ambako wanapelekwa katika vituo mbalimbali wakisubiri kurejeshwa kwao

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ni wakati ambapo hadhi ya ukimbizi ikisubiriwa kufutwa kwa Wanyarwanda ambao wangali uhamishoni katika pande zote za dunia, idara hii inawahimiza wakimbizi hawa kurejea wakati ambapo kuna baadhi yao waliokwisha chaguwa kuishi kwenye nchi za uhamisho na kuoana na wananchi wa hapo.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikiwahimiza wanyarwanda walioko uhamishoni kurejea kwa hiari. Serikali inatumia pia mbinu tofauti za kuwafanya wawe na hamu ya kurejea kwao, wanaorejea wanasaidiwa kuingizwa katika maisha ya kila siku kwa kupewa vifaa vya msingi, nyumba na vitu vingine vinavyotumiwa kama msaada wa msingi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.