kwamamaza 7

Umoja wa Ulaya yafuta mkutano wake wa kilele na Canada

0

Umoja wa Ulaya umeufuta mkutano wa kilele uliopangwa kuandaliwa leo kati yake na Canada, baada ya kushindwa kutatuliwa kwa muda ufaao mkwamo wa ndani unaoihusisha Ubelgiji kuhusu makubaliano ya kihistoria ya biashara huru kabla ya kutiwa saini na pande zote.

Serikali ya Ubelgiji imekuwa ikifanya juhudi za kuushawishi mkoa wa Wallonia wa kusini mwa nchi hiyo ambao wakaazi wake wanatumia Kifaransa kuunga mkono Makubaliano Mapana ya Kiuchumi na Kibiashara – CETA, ambayo yanalenga kuondoa vizingiti na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kati ya Canada na Umoja wa Ulaya kama vila hutangazwa dw Kiswahili.

Mkataba huo hauwezi kukamilika bila kuridhiwa na wanachama wote 28 wa Umoja wa Ulaya. Ujumbe wa Canada, ukiongozwa na Waziri Mkuu Justin Trudeau, haukwenda Brussels kama ilivyopangwa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.