Shilika la Umoja wa Mataifa (YUNA) linashtaki serikali ya Burundi kusaidia kundi la wanamgambo wanaosemekana kuwa ni wa Kayumba Nyamwasa, mpinzani mkubwa wa serikali ya Rwanda.

Ripoti  hii inasema kwamba Burundi inasaidia mno katika mambo ya kusajili wanajeshi kutoka nchini humo na kuwasaidia kufika eneo la Fizi, DR Congo na usafirishaji wa silaha.

Kiongozi mkubwa katika shughuli za kusajili anajulikana kwa majina ya  Rashid/Sunday ama Sundey Charles anayeishi mjini Bujumbura.

Ripoti inaeleza pia silaha zinasafirishwa kupitia eneo la Rumonge nchini Burundi kufika kwenye makao ya wanamgambo wa P5 huko Bijabo.

Ripoti ya YUNA inasema kwamba  hawa wanamgambo wanafanyia shughuli zao mashariki mwa DR Congo na kuwa mambo ya kusajili yanaendelea ndani na nje.

Kwa mujibu wa wataalamu wa YUNA, ambao walifanya hii ripoti, kwenye mazungumzo ya kipekee mwezi Septemba 2018, 12 waliokuwa katika hili kundi kila mmoja mwao  alisema kwamba linaongozwa na Shaka Nyamusaraba na kwamba washiriki wengi mwao ni wenye asili nchini Rwanda na jamii ya Wanyamulenge nchini DR Congo.

Taarifa hizi zinaeleza hili kundi linaitwa P5 na Kiongozi wake, Nyamwasa huzuru mala nyingi lili jimbo la mashariki mwa DR Congo.

Kwa upande mwingine, hawa wataalamu wa YUNA wamesema “ Hatuwezi kuhakikisha haya yote” kwani wanasubiri msaada wa Afrika Kusini kuhusu hili suala.

 

 

 

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.