kwamamaza 7

Umoja wa mataifa kutafuta nchi nyingine ya kukaribisha wakimbizi kutoka Israel badala ya Rwanda 

0

Shilika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi,UNHCR limetangaza kuwa kunatokea mahojiano kati yake na serikali ya Israel ili kutafuta nchi nyingine ambayo itawakaribisha wakimbizi badala ya Rwanda.

Shilika hili limetangaza haya baada ya siku mbili mahakama kuu kutangaza kwamba Rwanda haina viwango vya usalama kamili vya kuwakaribisha wakimbizi vliivyotolewa.

UNHCR jana imehakikisha kuwa mazungumzo haya yanalenga kuhojiana na Isreal kuhusu kuhamisha baadhi ya wakimbizi katika nchi nyingine ambayo Umoja wa Mataifa(YUNA) inasema kwamba ni “salama” kama ilivotangazwa na The Times of Israel.

Afisa kwa wajibu wa mawasiliano wa UNCHR,Sharon Harel ametangazia Jerusalem post kuwa inawezekana kuwa nchi ambayo itachukuwa nafasi ya Rwanda kukaribisha wakimbizi ni moja mwa zile zilizopiga hatua ya maendeleo pamoja na kuwapatia baadhi ya wakimbizi kuishi milele nchini Israel.

Pamoja na haya,Waziri wa mambo ya nje wa Israel  Tzipi Hotovely jumanne alimuonya Waziri mkuu Benjamin Netanyahu kwamba serikali haitaweza kufanya ufuatiliaji wa yatakayowafikia wakimbizi 20,000 asili ya Eritrea na Sudan iwapo mpango wa kuwahamisha utakuenda kama ulivyopangwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Mahojiano haya yakizaa matunda,inawezekana kwamba Israel itakoma kampeni za kuwahamisha wakimbizi nchini Uganda ama Rwanda”amesema Sharon Harel.

Hili ni baada ya maelfu ya wakimbizi kutoka Afrika kufanya maandamano nje ya ubalozi  wa Rwanda nchini Israel eneo  la Herzliya.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.