Swahili
Home » Umeme kusambazwa kwenye maeneo yote ya wilaya ya Karongi
HABARI SIASA

Umeme kusambazwa kwenye maeneo yote ya wilaya ya Karongi

Tatizo la umeme kushughulikiwa ikiwa kumekuwa na tarafa mojawapo zilizokuwa na umeme kwenye tara moja au mbili na kuna ahadi litakuwa limekwisha mwanzoni mwaka wa 2018.

Tarafa mojawapo kama Gishyita, Mubuga na Rwankuba ambazo zimekuwa na umeme kwenye tarafa moja au mbili tu zinaahidiwa kuwa zitakuwa na umeme siyo baada ya mwanzo wa mwaka ujao wa 2018.

Ni wakati ambapo waendashaji shughuli za kibinafsi hasahasa wanaoendesha biashara ya maduka wanaonyesha hamu ya kuwa na umeme.

Ndayishimiye mkazi wa eneo la Karibu na Rugabano kwenye kimji kidogo cha biashara cha Gitega amesema “swala la ukosefu umeme ni pingamizi kwa shughuli za eneo hili… unaona biashara mojawapo zinakwama hakuna atakayeweza kuendesha biashara ya kunyoa”

Uongozi wa wilaya ya Karongi unaeleza kuwa mradi wa kusambaza umeme kwenye maeneo yote ya Karongi umekwisha anza.

Ndayisaba François, meya wa wilaya ya Karongi alieleza kwamba shirika la kusambaza umeme(REG) limekwisha anza utaratibu wa kusambaza umeme kwenye maeneo yote na kwa hivyo tarafa zilizo kuwa na upungufu wa umeme zitajibiwa.

“REG inakaribia kusambaza umeme kwenye maeneo mengi yawezekanayo, kuna kampuni iliyopewa soko la kuasilisha miti ya kushikilia nyaya za umeme, kuna juhudi ya kuhakisha kila eneo linapata umeme”

makazi ya pamoja ya kisasa

Wakazi wa maeneo ya makazi ya pamoja wao watarahisishwa kupata umeme kwa kasi na wananchi wengine wanahimizwa kuhamia makazi ya aina hii.

Tarafa kama Mubuga ilikuwa na huduma ya umeme kwenye kata la Byaruhanga. Gishyita kwenye kata mbili. Na halafu Rwankuba kwenye kata moja tu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com