Swahili
Home » Ujerumani yamtuma nchini Rwanda Twagiramungu mtuhumiwa wa mauaji ya kimbali
HABARI

Ujerumani yamtuma nchini Rwanda Twagiramungu mtuhumiwa wa mauaji ya kimbali

Ujerumani inajianda leo kumtuma nchini Rwanda mtuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi  mwaka 1994,Jean Twagiramungu.Ni jambo amabalo alikataa mala nyingi kwa kutumia mahakama za huko Ulaya.

Akizungumza na The New Times,mwendesha mashtaka mkuu wa jamhuri,Jean Bosco Mutangana amaetangaza k kuwa Twagiramungu anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya tutsi 1994 sehemu za Gikongoro,mkoa wa kusini atafika nchini Rwanda leo.Mutangana amesema”Tuko tayari kumfanyia lolote kulingana na sheria kama watuhumiwa wengine,hii ni hatua ya njema ya kuwahukumu walioshiriki katika mauaji ya kimbali”.

Jean Bosco Mutangana amendelea kusema kuwa huu ni mfano bora wa kufuatilia na kuwa wataendelea kutafuta wahutumiwa popote wanapokificha dunia nzima na kunena”Nafikiri kuwa nchi nyingine zinahitaji kuiga Ujerumani.Kuna nchi nyingine barani uraya zilizojaribu haya kama vile Denmark,Norway, Holland,Canada na Marekani”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Jean Bosco Twagiramungu alikamatwa mjini Frankfurt mwaka 2015, Wenyeji wa kijiji alipokuwa akishi wakati wa mauaji ya kimbali wanasema kuwa mchango wake katika mauaji ya wengi kama mtu aliyekuwa mwalimu  ni kushawishi Interahamwe kuua watu na kuwapa silaha za kienyeji kama mipanga.Pia wanaongeza kuwa alionekana kwenye maeneo mbalimbali ya kuua watu madai ambayo Twagiramungu yakana mno.

Ni mala ya kwanza Ujerumani kumtuma mtuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi nchini Rwanda lakini kuna wengi  kama Onesphore Rwabukombe,Ignace Murwanshyaka na Straton Musoni waliokatiwa kesi na mahakama za Ujerumani.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com