kwamamaza 7

Uingereza yaiwekea masharti Rwanda ili iweze kuwapeleka wahalifu kwenye mahakama za Rwanda.

0

Kesi ya kuwapeleka wanyarwanda wanaotuhumiwa uhalifu katika mauaji ya kimbari yazidi kuwa vuta nikuvute baada ya Uingereza kuiwekea masharti Rwanda ya kutekeleza kabla ya kuwapeleka wanyarwanda watatu kusikiza kesi yao kwenye mahakama za Rwanda.

Kesi ya wanyarwanda hawa walikuwa watano kwa ujumla kabla ya  wengine wawili kuachiliwa huru wiki jana na uamuzi uliotupiliwa mbali na Serikali ya Rwanda.

Mahakama za Uingereza zilidai kwamba kwa kuwa kesi za wanyarwanda hawa ziliendeshwa bila kuwepo kwao kwa hivyo hivyo ingekuwa kuvunja sheria mara mbili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Masharti waliyowekewa Rwanda ni pamoja na mahakama za Uingereza kufadhili shughuli za upelelezi juu ya watuhumiwa, kuwapeleka mawakili kutoka nchi za kimataifa wenye uzoefu mkali na hata kuwa najaji kutoka nchi za nje kwenye jopo la majaji watakaoendesha kesi hiyo.

Rwanda inasema inaweza akayatekeleza masharti hayo lakini la mwisho ikasema ni mzigo kwakwe kama gazeti la The East African lililotangaza.

Wanyarwanda hao ambao wanashtumiwa uhalifu ni Celestin Mutabaruka na Emmanuel Nteziryayo, ambao waliachiliwa huru siku za hivi karibuni.

Wengine ambao mahakama ya Uingereze imesema huenda wasipewe haki stahiki na mahakama za Rwanda ni Celestin Mutabaruka na Emmanuel Nteziryayo, Mahakama hiyo ilisema pia kwamba iwapo Rwanda itakuwa tayari kukubali mabadiliko katika ngazi zake za kisheria basi nao watakubali matakwa yao.

Serikali ya Rwanda ilipendekeza kwamba kuwapeleka watuhumiwa hao kuja kusikiza kesi zao Rwanda ingekuwa hata kuwarahisisha Wanyarwanda kufuata kesi zao hususani waathirika.

Rwanda imewekewa siku ya mwisho hadi tarehe 18 Agosti kueleza ikiwa iko tayari kutimiza masharti hayo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.