kwamamaza 7

Uingeleza: Watuhumiwa 5 wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi katika mahakama ya rufaa

0

Wanyarwanda tano ambao wanatuhumiwa kushirika katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yaliofanyika mnamo 1994, watafikishwa mahakamani nchini Uingeleza ili kusikilizwa kuhusu kuhamishwa kwao nchini Rwanda walipofanyia dhambi.

Wanaotuhumiwa ni Vincent Bajinya aliyekuwa mganga, Celestin Mutabaruka aliyekuwa mchungaji katika dini na wengine wa tatu ambao walikuwa meya yaani Celestin Ugirashebuja, Charles Munyaneza na Emmanuel Nteziryayo.

Mahakama nchini Uingereza anasikiliza kwa upya kesi ya rufaa iliyowakilishwa na serikali ya Rwanda dhidi ya watuhumiwa hawa wanaoshitakiwa kushiriki mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa kabila la kitutsi nchini Rwanda na watu zaidi ya milioni moja wakapoteza maisha.

Mwaka uliopita Mahakama ya Westminister magistrate lower court alitupilia mbali ombi lililotolewa na serikali ya Rwanda la kuhamisha nchini Rwanda waume tano wakisema kwamba wanaweza kunyimwa haki ya kisheria baada ya kufikishwa katika mahakama ya Rwanda.

[ad id=”72″]

Kesi hii inasikilizwa kwa upya kufuatia rufaa iliyotolewa na serikali ya Rwanda mahakamani ya Royal Court of Justice nchini humo dhidi ya washukiwa hao.
Hawa watano walikamatwa katika maeneo tofauti nchini Uingereza kutokana na nyaraka za kuwakamata zilizotolewa na mahakama ya Rwanda.

Taarifa iliotolewa na shirika la walionusulika mauaji ya kimbari ya 1994 linalokuwa nchini Uingeleza, Urumuri; huonyesha msiba kwa sababu ya kuacha huru watuhumiwa wakati walionusulika mauaji ya kimbari wangali wakiumizwa na matokeo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.