Mawakili wawili Juan de Dios Crespo na Marco Motta walijaribu asubuhi ya leo kuasilisha kitita cha fedha ya kutengua kifungu cha uhamisho wa Neymar cha €222 m(198)  kwenye uongozi wa La Liga ili kumruhusu nyota huyo kuhamia kwenye klabu ya Ufaransa.

Hata hivyo matumaini ya PSG kumchukua Neymar hayakuenda haraka iwezekanavyo baada ya La Liga kukataa kuikabidhi fedha ya kununua kandarasi ya Neymar kwenye klabu ya Barcelona.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rais wa La Liga Javier Tebas, amethibitisha habari hizi kwa kusema “ningependa kuhakikisha kwamba  mawakili wa mchezaji huyo wamefika asubuhi ya leo kwenye ofisi ya La Liga wakileta fedha ya kutengua kifungu cha uhamisho wa Neymar na kwamba fedha hiyo haikupokewa”

Ameongeza “hizo ndizo habari tunazoweza kutoa kwa sasa”.

Rais huyu amedai kwamba uhamisho huo ungeweza kuhusika na ukiukaji wa kanuni za fedha za UEFA(FFP) na kwamba anapaswa kuzilinda kalabu kubwa za Uhispania juu ya matatizo kama hayo.

Inasemekana kuwa pia La Liga ina mashaka kuhusu asili ya kitita cha fedha ya uhamisho huo na kwamba kulingana na kanuni za La Liga timu za uhispania ndizo zinazo haki ya ununuzi wa kandarasi. Thamani ya dili ya Neymar itakuwa jumla ya milioni 450 za pauni.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.