kwamamaza 7

Uganda:Waziri wa mambo ya nje abadili maneno yake husika na taarifa za mkutano kati ya Rais Kagame na mwenzake,Museveni

0

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda,Oryem Okello amebadilisha maneno yake aliyotangazia vyombo vya habari nchini Uganda kuwa Rais Kagame alikutana na kuzungumza na mwenzake wa Uganda,Yoweli Museveni walikohudhuria mkutano mjini Dubai,Umoja wa falme za kiarabu.

Waziri Oryem amesema kuwa hakumanisha kuwa kulikuwa mazungumzo kamili ila marais wawili hawa walikutana na kusalimiana na kuwa kitendo hiki kinamaanisha kuwa kuna ushirikiano mzuri kati ya Rwanda na Uganda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya ikulu ya Rwanda siku moja kabla kupitia afisa wa mawasiliano,Yolande Makolo kutangaza kuwa haukuweko mkutano kati ya Rais Museveni na Rais Kagame.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hatimaye,kuna taarifa kuwa kuna vita baridi kati ya nchi hizi mbili juu ya mambo ya usalama,upelelezi na kutotimiza ahadi mablimbali za miradi ya maendeleo kama vile miundo mbinu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.