kwamamaza 7

Uganda:Wanyarwanda wakamatwa kwa kutuhumiwa kuwa wapelelezi

0

Wanyarwanda karibu elfu moja wamekamatwa na kufungwa jela nchini Uganda baada ya kutuhumiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Baadhi yao 350 ni wafungwa gerezani Kisoro, 420 gereza ya Kabale na wengine 180 ni wafungwa kwenye gereza kuu ya Ruzira,mjini Kampala.

Kwa upande mwingine kunadaiwa kuwa Wanyarwanda hawa walikuenda nchini Uganda kuwatembelea ndugu na marafiki,kutafuta kazi na mengine kinyume na kuwa wapelelezi wa Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wengi mwa hawa walikamatwa kwa kuwa walikuwa hawana vitambulisho rasmi,Mnyarwanda mmoja aliyewahi kukamatwa mjini Kampala,Faustin Habimana,27,ametangazia Bwiza.com kuwa alikamatwa  baada ya kumaliza siku nne mjini Kampala ila alikuwa na kitambuisho cha miezi mitatu,jambo lililomsikitisha mno.

Habimana amesema kuwa aliachiwa huru baada ya kumpigia simu nduguye aliyekuwa nchini Rwanda ili kumletea shilingi miliyoni mbili,jambo lililombidi kuuza shamba lake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya taarifa kadhalika za vyombo vya habari nchini akama vile Chimpreports kutangaza kuwa kuna vita baridi kati ya Rwanda na Uganda juu ya upelelezi na kuwateka nyara wakimbizi na sababu za kiuchumi na mengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.