kwamamaza 7

Uganda:Wanyarwanda kuendelea kufungwa jela kwa sababu ya serikali kukosa fedha za kufanya upelelezi

0

Mahakama mjini Mbarara imeamua kuendelea kuwafunga jela  watu  45 wakiwemo Wanyarwanda 36 hadi tarehe 5 Februari 2018  juu ya mashtaka ya vitendo vya ugaidi kutokana na kuwa serikali haina fedha za kutosha ili kufanya upelelezi.

Mahakama imeamua hili kufuatia ombi la mwendeshamashtaka Anthony Ulijishuli la kuwa kunahitajika muda wa kutosha ili serikali iweze kumaliza upelelezi kuhusu suala hili.

Ulijishuli  ameweka wazi kwamba upelelezi ulichelewa kutokana na ukosefu wa fedha.

Mwanasheria wa washtakiwa Innocent Okong amesema kuwa suala la ukosefu wa fedha haliwahusu watuhumiwa ila linahusu serikali au gereza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Innocent Okong ameongeza kuwa serikali ingelijua hili isingeliwakamata

Huyu amesisitiza kuwa hawa Wanyarwanda walikuwa wakielekea nchini Tanzania katika shughuli za kidini  siyo vitendo vya ugaidi kama inavyoeleza serikali.

Jaji Ayebare ametoa amri ya kuwafunga gerezani Kyamugorani mjini Mbarara kinyume na kuwarudisha Nalufenya,wilayani Jinja.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.