kwamamaza 7

Uongo mtupu wa msemaji wa polisi ya Uganda husika na wakimbizi asili ya Rwanda wajulikana

0

Uongo wake msemaji wa Polisi ya Uganda,Emilian Kayima umejulikana baada ya taarifa tofauti na zile alizotangaza siku zilizopita kama sababu iliyowafanya wakimbizi asili ya Rwanda waliokuwa wanatarajia kujulisha suala la kutekwa nyara bungeni kutotimiza jambo hili, kutangazwa.

Emilian Kayima alitangazia Chimpreports kuwa wakimbizi hawa hawakuweza kufika bungeni kwa kuwa waziri wa usalama,Luteni Jenerali Henry Tumukunde alikuwa hayupo nchini na kwa hiyo itabidi kumngoja atakaporudi.

Kwa upande mwingine,taarifa za The Standard  zinasema kuwa ombi la wakimbizi asili ya Rwanda lilipigwa marufuku kwa kuwa lilikuwa ni uongo mtupu.Taarifa hizi zinasema kuwa maneno yake Kayima ni uongo kwa kuwa ombi hili husika na bunge huwasilishwa kwa spika siyo waziri.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya taarifa za Chimpreports kutangaza kuwa wakimbizi hawakufika bungeni kama ilivyotarajiwa kutokana na kuwa walishambuliwa huko eneo la Ntinda, mjini Kampala walipokuwa wakijianda kuenda bungeni kama mmoja wao alivyotangazia chombo cha habari hiki.

Wakimbizi asili ya Rwanda walikuwa wakitaka kujulisha bunge la Uganda kuwa wana wasiwasi nyingi kutokana na utekanyara wanaofanyiwa na mafisa wa upelelezi wa serikali ya Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.