kwamamaza 7

Uganda:Polisi yatoa ulinzi mkali kwenye kaburi ya marehemu Mowzey Radio

0

Polisi mjini Kampala nchini Uganda imeweka wazi kutoa ulinzi mkali kwenye kaburi ya marehemu muimbaji Moses Ssekibogo Nakitinje maarufu kama Mowzey Radio na kwa familia yake kutokana na vitisho vya mashambulizi vya watu ambao hawajajulikana.

Msemaji wa polisi mjini Kampala,Luke Owesigyire ametangaza kwamba wamepokea ripoti ya familia hii ikisema kwamba kuna watu wanaoahidi kuwavamia wasipochimba kaburi ya marehemu au kuuza baadhi ya mali ya Radio ili kuwapatia gao lao.

“Mama wa Radio ametuambia kuhusu watu ambao wanambabaisha kimwili na kupitia simu.Amefichua kuwa kuna yule ambaye anajidai kuwa ni baba wa Radio”Luke Owesigyire amesema.

Afisa huyu ameshauri anayedai kuwa ni baba wa marehemu kutumia mbinu za sheria kma anataka kaburi ya marehemu kuchimbwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa hili,Kituo cha polisi cha Kajjansi kimeamua kutoa ulinzi kwenye kaburi ya Mowzey Radio.

Mama wa Radio,Kasuubo Jane na ndugu ye Eddy Sembajwe wametangazia Chimpreports kwamba vitisho hivi vilianza alhamisi wiki iliyopita baada ya taarifa kuenea kwamba muimbaji Mowzey Radio ameaga dunia.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.