kwamamaza 7

Uganda:Polisi yachunguza vitambulisho vya Wanyarwanda waliokamatwa

0

Polisi ya Uganda imeweka wazi kufanya uchunguzi wa vitambulisho vinavyosemekana kuwa “bandia” vya Wanyarwanda 40 waliokamatwa kwenye mpaka wa Uganda na Tanzania,Kikagati.

Msemaji wa polisi ya Uganda,Emilian Kayima ametangazia Chimpreports kuwa wakimbizi hawa wanahojiwa kuhusu hili kwa kujua mapana na marefu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia amesema kuwa wanalolijua ni kwamba wakimbizi hawa walibebwa na gari la Uganda wakielekea nchini Burundi kwa shughuli za ukristo.

Kwa upande mwingine, chombo cha habari  Virunga post kiliandika kuwa Wanyarwanda hawa walikuwa wakielekea nchini DR Congo kufanya mafunzo ya kijeshi ya chama cha upinzani wa serikali ya Rwanda ( RNC),madai ambayo msemaji wake Jean Paul Turayishimiye amekanusha mno.

Kayima amendelea kueleza  kuwa hawa walirudishwa nchini Uganda ili kujua ukweli ama uongo wa vitambulisho vyao.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,Kayima ameongeza kuwa hawa watadhibiwa kulingana na sheria watakapokuwa na hatia na kusisitiza kwamba watajulisha dunia nzima yote husika na kisa hiki wakati utakapofika.

Haya ni baada ya taarifa za vyombo vya habari nchini Uganda hivi karibuni kutangaza kuwa kuna vita baridi kati ya Rwanda na Uganda juu ya upelelezi,kuwateka nyara wakimbizi na mengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.