Home HABARI MPYA Uganda:Mnyarwanda Rene Rutagungira asimama kizimbani kwa kumteka nyara aliyekuwa mlinzi  wa Rais Kagame
HABARI MPYA - SIASA - October 28, 2017

Uganda:Mnyarwanda Rene Rutagungira asimama kizimbani kwa kumteka nyara aliyekuwa mlinzi  wa Rais Kagame

Mnyarwanda Rene Rutagungira ameonekana mahakamani ya kijeshi,Makindye akihojiwa kuhusu uhalifu wa kumtaka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame,Luteni Joel Mutabazi.

Haya ni baada ya taarifa zilizoenea terehe 8 Ogasti kuwa Rutagungira ametoweka.Huyu anatuhumiwa kushiriki katika kisa cha kumrudisha Luteni Mutabazi aliyehukumiwa kufungwa maisha jela na mahakama ya kijeshi nchini Rwanda.

Akisoma kesi hii, Mkuu wa mahakama Luteni Generali Andrew Gutti ameleza kuwa alifanya kitendo kilicho kinyume na sheria ya kuadhibu makala ya 242 cha kumteka nyara Mutabazi na kumtuma nchini Rwanda alipokuwa eneo la Mpigi,akiwa na bunduki na grunedi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za Chimpreports zinaeleza kuwa haijajulikana kwa nini kuna polisi wa uraia wa Uganda katika kesi hii ila inahusishwa na taarifa za kuwa Rais Kaguta Museveni alipokea barua ya Umoja wa Mataifa ilimjulisha kuwa anapaswa kufanya kitu Fulani kwa kuzuia mateso ya Wanyarwanda nchini Uganda anayofanywa na polisi ya nchi yake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rene Rutagingira alikuwa mwanajeshi wa Rwanda,anaishi nchini Uganda na taarifa zinasema kuwa kisa hiki kinaweza kuzusha kutoelewana kati ya Rwanda na Uganda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Phillipe Nsengiyumva/Bwiza.com

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.