kwamamaza 7

Uganda:Mnyarwanda atekwa nyara mjini Mbarara

0

Mnyarwanda Emmanuel Cyemayire alitekwa nyara na maafisa wa usalama ambao hawajatambulika  jana alipokuwa magharibi kusini mwa nchi,mjini Mbarara.

Bw Emmanuel Cyemayire alitekwa nyara baada ya maafisa wa usalama wenye bunduki kumuomba kuingia garini kisha wakaondoka mahali ambapo hapakujulikana kwa mashahidi.

Shahidi mmoja  wa jambo hili ametangazia Chimpreports kuwa Cyemayire ni mwenyeji wa duka mjini Mbarara na kuwa alipelekwa mahali amabapo hawakujua.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za Chimpreports zinasema kwamba bin Cyemayire amewasilisha suala hili kwenye kituo cha polisi cha Mbarara ila polisi imejibu kuwa  Cyemayire hayupo gerezani.

Hili ni baada ya waziri wa mambo ya nje wa Uganda,Sam Kutesa ijumaa kumkuta na kujadiliana na Rais wa Rwanda,Paul Kagame kuhusu masuala ya kuboresha ushirikiano unaotumbukia nyongo kati ya nchi hizi.

Pia ni baada ya Uganda kujibu Rwanda kuwa Wanyarwana wanaokamatwa nchini Uganda ni wale ambao wenye uhusiano na mambo ya vitendo vya ugaidi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na Twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.