Swahili
Home » Uganda:Mnyarwanda akamatwa  kwa kusajili wanamgambo wa kuipindua serikali ya Rwanda
KIMATAIFA

Uganda:Mnyarwanda akamatwa  kwa kusajili wanamgambo wa kuipindua serikali ya Rwanda

Wanausalama wilayani Kakumiro wamemkamata Mnyarwanda Dioden Kabanda, 32 ambaye anatuhumiwa vitendo vya kusajili wanamgambo wa kuipindua serikali ya Rwanda.

Mtuhumiwa alikamatwa terehe 4 Januari 2018 alipokuwa baani Legacy kijijini Mapasana.

Kabanda alikuwa akiwaomba  Wanyarwanda kutoa msaada wa shilingi 5000 kwa kutoa risiti ya Chama cha ‘Rwanda Democratic Party’ kulingana na muhuri ya risti.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Spyreports imetangaza kwamba huyu huyu alikuwa akitoa ahadi kwamba hawa Wanyarwanda waliolipa atawarudisha nchini Rwanda kuipindua serikali.

Kuna taarrifa kwamba kiongozi wake anaishi nchini Burundi na kuwa kuna mwingine kwa jina la Rugamba ambaye anaishi katika kambi ya ukimbizi ya Nakivale wilayani Isingiro.

Dieden Kabanda ni mkazi wa kijiji cha Tegula,tarafa ya Nkooko wilayani Kakumiro.Kwa sasa angali mikononi mwa Wanajeshi kwa ajili ya upelelezi.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com