kwamamaza 7

Uganda:Maafisa wa upelelezi wahusiana na kumteka nyara Mnyarwanda Cyemayire

0

Maafisa wa Upelelezi wa Uganda,CMI  wamehusishwa na kitendo cha kumkamata Mnyarwanda,Emmanuel Cyemayire ambaye alitekwa nyara akiwa mjini Mbarara usiku wa tarehe 4 Januari 2018.

Taarifa za Virunga Post zinasema kwamba kabla  ya kitendo cha kumkamata Cyemayire,afisa mmoja wa upelelezi  Major Fred Mushambo ambaye ni kiongozi wa CMI katika eneo la Mbarara alifika anapoishi Cyemayire ila  Cyemayire hakukuwa nyumbani kwa kuwa alikuwa kazini dukani mjini Mbarara.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia taarifa hizi zinaeleza kwamba kuna mwinjilisti,Deo Nyirigira ambaye ni mwenyekiti wa kanisa la AGAPE mjini Mbarara aliyeshiriki katika kitendo hiki na kuwa kuna ushirikiano kati yake na chama cha Rwanda national Congress,RNC katika vitendo vya kuwakamata Wanyarwanda nchini Uganda kwa msaada wa CMI.

Ikumbukwe kwamba maafisa wa upelelezi nchini Uganda mala nyingi  walishtakiwa  kuwateka nyara na kuwatesa kimwili mno Wanyarwanda wakiwemo Fidele Gatsinzi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.