Swahili
Home » Uganda:Kanisa lageuka kiota cha kusajili wanajeshi wa RNC
HABARI MPYA

Uganda:Kanisa lageuka kiota cha kusajili wanajeshi wa RNC

Mwenyekiti na kiongozi wa RNC,Jenerali Kayumba Nyamwasa

Taarifa zimezagaa kwamba kanisa la AGAPE wilayani Mbarara ni kiota cha kusajili wanajeshi wa chama cha upinzani kwa serikali ya Rwanda,Rwanda National Congress,RNC kinachoongozwa na Jenerali Kayumba Nyamwasa.

Kwa mujibu wa taarifa za Virunga Post,kanisa hili la mwinjilisti Deo Nyirigira ndilo linalowasidia wanachama wa RNC katika mipango yao ya kusajili na kupanga vilivyo operesheni zao kama vile kuorodhesha Wanyarwanda ambao ni vipingamizi kwa mipango yao, eneo la magharibi ili wakamatwe kwa kuwaita wapelelezi wa Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Shahidi mmoja ametangazia hiki chombo cha habari kuwa mala nyingi Wanachama wa RNC hufanya mikutano kanisani chini ya kivuli cha kuwa katika shughuli za kidini.

Pamoja na hili, bin mwinjilisti Deo Nyirigira,Felix Mwizerwa anahusishwa kuwa baadhi ya watu waliosajili na kusindikiza Wanyarwanda 43 waliokamatwa kwenye mpaka kati ya Rwanda na Uganda,Kikagati wakielekea nchini Burundi kisha yeye akatoroka baada ya kuona kwamba polisi ya Uganda imewakamata.

Mwinjilisti Deo Nyirigira alikimbilia nchini Uganda mwaka 2000 baada ya kushtakiwa unyonyaji kwa waliokuwa wakristo wa kanisa lake.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com