Rugema kayumba

Mwanaume aliyesikika mara nyingi akishtakiwa kuwateka nyara Wanyarwanda nchini Uganda,Rugema Kayumba,40, aliwahi kuwa mwanajeshi wa Rwanda.

Kwa mjibu wa taarifa za Virunga post,Rugema Kayumba alizaliwa nchini Uganda na kusoma shule la msingi Bujaburi 2 wilayani Tooro,alisoma shule ya sekondari nchini Uganda na Rwanda,kisha akasajiliwa katika jeshi la Rwanda,RDF kwa cheo cha Kopolo(Corporal).

Pia alisoma chuo kikuu cha Kigali Institute of Science and Technology (KIST) na kupata shahada katika kitivo cha sayansi ya vyakua(Food Science) mwaka 2005.

Baada ya masomo yake alijiunga tena na jeshi kisha akajiuzulu na kukimbilia nchini Uganda.

Taarifa hizi zinasema kuwa maisha yake yalikuwa magumu hadi alipoenda nchini Iraq kufanya kazi ya ulinzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baada ya mkataba wa kazi ya ulinzi kumalizika,Rugema Kayumba alienda nchini Norway na kuishi mjini Oslo kisha akarudi nchini Uganda alipoanza kazi ya uunganishi wa operesheni za RNC.

Rugema Kayumba ambaye ni mpwa wa Jenerali Kayumba nyamwasa,alishtakiwa kumteka nyara Mnyarwanda Fidele Gatsinzi ambaye aliachiwa huru na kutupwa kwenye mpaka wa Katuna baada ya kuteswa kimwili mno na maafisa wa upelelezi wa Uganda,CMI.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.