kwamamaza 7

Uganda yatuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu Rais Kagame

0

Baada ya taarifa za kuwa kuna vita baridi kati ya Rwanda na Uganda,kumeibuka fununu ambazo zinaenezwa na vyombo vya habari nchini Uganda kuhusu Rais wa Rwanda,Paul Kagame.

Haya ni baada ya taarifa zilizojulikana kuwa uongo za The New Vision zilizoeleza kuwa Rais Kagame na mwenzake wa Uganda,Museveni walikutana mjini Dubai,madai yaliyokanushwa mno na ikulu ya Rwanda kwa kusema kuwa hili halikutokea.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia moja mwa vyombo vya habari vya upinzani wa serikali ya Rwanda viliandika kuwa Rais Kagame aliwaita mafisa wakuu wa usalama mwishoni mwa wiki iliyopita Taarifa zinazotuhumiwa kuwa ni asili ya serikali ya Uganda.Taarifa za News of Rwanda zinasema kuwa hizi ni fununu kwa kuwa Rais Kagame baada ya mkutano wa ‘Africa Global Business Forum punde si punde alielekea nchini Uingereza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za The News of Rwanda zinaleza kuwa vitendo vya Uganda vya kusambaza fununu vinalenga kuwachanganya watu ili wasiendele na ufuatiliaji wa ghasia za kisiasa zilizoko.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.