kwamamaza 7

Uganda yakanusha taarifa za kudhamiria kuipindua serikali ya Rwanda

0

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda,Amb.Patrick S. Mugoya jana amekanusha taarifa za baadhi ya vyombo vya habari nchini Uganda za kuwa Uganda inahusika mpango wa kupindua utawala wa Rais Kagame.

Chombo cha habari kimoja nchini Uganda kimeweka wazi chombo cha habari nchini Rwanda kilichotangaza kuwa serikali ya Uganda ina mpango wa kupindua serikali ya  Rwanda.

Waziri Amb. Patrick S. Mugoya jana tarehe 20 Novemba 2017 amekanusha taarifa hizi na kusisitiza kuwa kuna ushirikiano mzuri kati ya Rwanda na Uganda.

Waziri Mugoya amesema”Wizara inawajulisha wakazi wa raia wa Uganda na Rwanda kuwa taarifa za Rushyashya na Redpepper na vyombo vya habari vingine (…) zinadhamiria kuchochea na kuharibu ushirikiano kati ya nchi zetu”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri huyu amendelea kusema kuwa amepiga marufuku matumizi ovyo ya uwanja wa kuwasilisha habari.

Baadhi ya taarifa zilizojulikana ni zile zilizokuwa zikisema kuwa ndugu yake Rais Museveni,Gen.Caleb Akandwanaho maarufu kama Salim Saleh na Waziri wa usalama wa ndani,Gen.(Rtd) Henry Tumukunde pamoja na Jenerali raia wa Ufaransa walizungumza na Rais Museveni kuhusu namna ya kushambulia Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Juu ya haya,Waziri wa mambo ya nje wa Uganda ameongeza kuwa hakuna serikali kati ya Rwanda  na Uganda iliyowahi kuongea kuhusu suala hili kupitia mbinu za kawaida zinazotumiwa na viongozi na kwa hiyo wizara anayoiongoza haiwezi kutangaza yaliyo kinyume na hali ya mambo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri huu ametangaza haya  wakati ambapo taarifa za vingi mwa vyombo vya habari nchini Uganda vilitangaza  kuwa kuna vita baridi kati ya Rwanda na Uganda juu ya upelelezi,kukamatwa kwa wakimbizi,kutotimiza miradi mbalimbali ya maendeleo na mengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.