kwamamaza 7

Uganda yajibu Rwanda kuhusu vitendo vya kuwakamata Wanyarwanda

0

Serikali ya Uganda imejibu serikali  ya Rwanda kuhusu vitendo vya kuwakamata Wanyarwanda mbalimbali nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa za Chimpreports, serikali ya Uganda imeweka wazi kwamba Wanyarwanda waliokamatwa na kufikishwa mahakamani ni wale ambao wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano na vitendo vya ugaidi nchini Uganda.

Hata kama katibu mkuu kwenye wizara ya mambo ya nje ya Uganda,Amb.Patrick Mugoya angali likizoni,taarifa hizi zimesema kwamba atatangaza mengi zaidi kuhusu hili wakati ukifika.

Pamoja na haya,wafuatiliaji wa visa vya kuwakamata Wanyarwanda nchini Uganda wamesema bila kusita kwamba ni lazima kuadhibu wahalifu kulingana na sheria.

Hili ni baada ya ubalozi wa Rwanda kutumia barua Uganda kwa kutaka kujua mapana na marefu husika na vitendo vya kuwakamata vilivyokuwa wikiwakabili Wanyarwanda nchini Uganda.

Ushirikiano kati ya Rwanda ulianza kuenda goigoi mwaka jana 2017 baada ya taarifa zilizoenea kwamba kuna vita baridi kati ya nchini hizi juu ya upelelezi,kuwateka nyara wakimbizi,kutotimiza ahadi ya miradi ya kiuchumi na mengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na Twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.